Kocha Mkuu wa Al Ahly - Marcel Koller amekosoa upangaji wa ratiba ya Ligi ya mabingwa Afrika (CAFCL), akidai wachezaji wake wataathirika kutokana na msongamano wa mechi.

Mashindano mapya ya vilabu bora barani Afrika yataanza Oktoba 20 huku timu nane zilizofanikiwa zaidi barani humo zikipigania dola milioni 4 kwa ofa kwa washindi.

The Red Eagles Al Ahly watamenyana na Simba Sc ya Tanzania katika robo fainali, huku mkondo wa kwanza ukifanyika Dar es Salaam kabla ya kwenda Cairo kwa mkondo wa pili siku nne tu baadaye.

Huku mapumziko ya kimataifa ya Oktoba yakimalizika siku chache kabla ya AFL kuanza, Koller ana shaka kama ataweza kuchezesha kikosi kamili dhidi ya Wekundu hao wa Msimbazi.

You Might Also Like

Get Newsletter

Advertisement