Kiungo wa kati wa Manchester United Kobbie Mainoo ameitwa kwa mara ya kwanza kwenye kikosi cha Timu ya Taifa ya Uingereza kwa ajili ya mechi zijazo za kirafiki dhidi ya Brazil na Ubelgiji.

Mainoo mwenye umri wa miaka 18 awali aliitwa katika kikosi cha vijana chini ya umri wa miaka 21 lakini amepandishwa kwenye kikosi cha wakubwa cha Gareth Southgate.


England itacheza na Brazil Jumamosi ya mwishoni mwa wiki hii huku mchezo dhidi ya Ubelgiji ukichezwa Machi 26 ambapo mechi zote mbili zitapigwa huko Wembley.

Hizi zitakuwa mechi zao za mwisho kabla ya Southgate kutaja kikosi chake kwa Euro 2024.

Kwa upande wa Mshambulizi wa Newcastle Anthony Gordon na mlinzi wa Everton Jarrad Branthwaite walikuwa miongoni mwa wachezaji waliofika St George's Park baada ya kuitwa kwa mara ya kwanza katika kikosi hicho cha Timu ya wakubwa huku mshambuliaji wa Brentford, Ivan Toney akiwa anashiriki kwa mara ya kwanza tangu amalize kifungo cha miezi minane mara baada ya kukiuka sheria za Shirikisho la Soka (FA) kwa kujihusisha na mchezo wa kamari.

You Might Also Like

Get Newsletter

Advertisement