Jurgen Klopp alimsifu Alexis Mac Allister kwa "bao lake la ajabu" lililoisaidia Liverpool kushinda dhidi ya Sheffield United na kudhibiti mbio za kuwania taji la Premier League.

Blades waliomo mkiani mwa jedwali walikuwa kwenye sare ya kushtukiza kwenye Uwanja wa Anfield mapema, lakini Mac Allister - mshindi wa Kombe la Dunia akiwa na Argentina - alifunga bao zuri la umbali wa yadi 20 na kuwafanya Wenyeji hao kuwa mbele kwa mabao 2-1. .

Cody Gakpo aliongeza bao la tatu dakika ya 90 huku Liverpool ikirejea kileleni mwa jedwali.

Klopp alisema: "Tulihitaji bao la ajabu la Macca ili kugeuza hali. Ni muhimu sana kwetu, kwa kweli ni mchezaji mzuri - nina furaha sana kwa Liverpool kwamba tumempata.

"Kazi yake ya ulinzi imekuwa nzuri sana ambapo watu walikuwa wanamtilia shaka kama angeweza kulinda, lakini ninampendelea sana katika safu ya mbele ya kiungo cha kati’’.





You Might Also Like

Get Newsletter

Advertisement