KLABU ZA SOKA EPL ZIMEOMBWA KUUNGA MKONO PENDEKEZO LA KLABU YA WOLVERHAMTON HOJA YA KUPIGA KURA YA KUFUTA MATUMIZI YA VAR
Klabu zinazoshiriki Premier League zimeombwa kuunga mkono hoja iliyowasilishwa na Klabu ya Wolverhampton Wanderers inayopendekeza azimio la kupiga Kura ya kufuta Matumizi ya 'VAR' kuanzia Msimu ujao
Pendekezo hilo ambalo linadaiwa kupingwa na Bodi ya Ligi Kuu linatarajiwa kusikilizwa Juni 6, 2024 ambapo imeelezwa Bodi inatambua haki ya Wolves kutoa pendekezo hilo, lakini inadhani kufutwa kwa VAR kunaweza kusababisha maamuzi mengi yasiyo sahihi
Aidha, baadhi ya Maafisa wa EPL wanadai pendekezo hilo litaathiri Ubora wa Ligi, pia kwa mujibu wa takwimu za Msimu huu zinaonesha kiwango cha maamuzi sahihi ya Uwanjani kimeongezeka kutoka 82% hadi 96 kupitia VAR