Timu za Ligi Kuu ya nchini Sudan, Hay Al Wadi na Al Hilal FC zimefuzu kwa hatua ya mtoano kwenye michuano ya CECAFA Dar Port Kagame Cup 2004 nchini Tanzania.

APR FC kutoka Rwanda ndio timu ya kwanza kufuzu kwa nusu fainali mapema leo baada ya kutoka sare ya 1-1 dhidi ya SC Villa (Uganda) kileleni mwa Kundi C.

Kundi A Hay Al Wadi walitoka sare ya 1-1 dhidi ya Coastal Union FC katika mchezo uliopigwa kwenye Uwanja wa Azam Complex, Chamazi ambapo ushindi huo umeifanya Hay Al Wadi kufikisha pointi 7, huku Coastal Union ikimaliza nafasi ya pili ikiwa na pointi 4.

Dekedaha FC ya Nchini Somalia ilipata ushindi wake wa kwanza katika michuano hiyo kwa kuwafunga mabingwa wa Ligi Kuu ya Zanzibar, JKU SC kwa mabao 2-1.

Mechi za mwisho za Kundi C zitachezwa hii leo kwa ASAS Djibouti Telecom itamenyana na wageni Red Arrows FC kutoka Zambia, Al Hilal (Sudan) ambao tayari wamefuzu baada ya kuambulia pointi 6 watacheza dhidi ya Gor Mahia FC (Kenya).

SC Villa ya Uganda ambao wana pointi 5 watakuwa na matumaini kwamba Red Arrows watashindwa au kuchagua sare ikiwa wanataka kufuzu kwa hatua ya mtoano kama mshindi wa pili bora.

Ni Timu moja kwa kila kundi ndizo zitakazofuzu kwenda hatua Nusu Fainali huku kundi lenye matokeo bora zaidi likitoa timu mbili kwa maana ya timu kiongozi na Best Looser kwaajili ya kukamilisha idadi ya timu nne zitakazocheza Nusu Fainali ya Michuano hii ya CECAFA Dar Port Kagae Cup 2024.

Bingwa wa Michuano hii atajinyakulia kitita cha Dola za Marekani 30,000 huku timu itakayoshika nafasi ya pili ikiondoka na Dola 20,000 na wa tatu Dola 10,000.

You Might Also Like

Get Newsletter

Advertisement