Mabao matatu yaliyofungwa na mshambuliaji Kenedy Musonda, Clement Mzize na kiungo mshambuliaji, Mudathiri Yahya yametosha kuipa Yanga ubingwa wa tatu mfululizo Ligi Kuu Bara wakiichapa Mtibwa Sugar.


Yanga imeibuka na ushindi wa mabao 3-1 katika mchezo wa Ligi Kuu Bara uliochezwa leo Mei 13, 2024 katika Uwanja wa Manungu Complex uliopo Turiani mkoani Mogogoro.

Mchezo huo uliokuwa muhimu pia kwa Mtibwa wa kujinasua kushuka daraja na Yanga kutaka kutangazwa kuwa mabingwa msimu wa tatu mfululizo.

Matokeo hayo yamekuwa kitanzi zaidi kwa Mtibwa Sugar ambapo katika michezo 27 wamekusanya pointi 20 na kuendelea kusalia mkiani mwa ligi.


You Might Also Like

Get Newsletter

Advertisement