Klabu ya Yanga imemkabidhi 'uzi' wake Rais wa Shirikisho la Soka Nchini, Wallace Karia ambao atauvaa siku ya Jumamosi kwenye mchezo dhidi ya Mamelodi Sundowns utakaopigwa Benjamin Mkapa.

Imesalia wiki moja kuelekea mchezo huu ambao utafanyika tarehe 30/03, kwa upande wa Uongozi wa Yanga Sc, kupitia Afisa habari Ali kamwe alitangaza wataanza hamasa kuanzia wiki ijayo. 

Bado taarifa zakurejea kwa Pacome Zouzou na Yao kwasi Attahoula zipo 50/50 kuwepo katika mchezo wa Mamelodi Sundowns. 

Habari njema kwa mashabiki wa Yanga Sport Clubs wataruhusiwa kuingia uwanjani bure kwa wale watakaoingia majukwaa ya mzunguko.

You Might Also Like

Get Newsletter

Advertisement