Klabu ya Young Africans iliyoko Ligi Kuu ya NBC imefungiwa kufanya usajili kwa kukiuka kanuni za Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA).

Uamuzi huo umefanywa na FIFA baada ya klabu hiyo kukiuka Annexe 3 ya Kanuni ya Uhamisho wa Wachezaji (RSTP) ya Shirikisho hilo.

Pamoja na masuala mengine, Young Africans haikuingiza uthibitisho wa malipo ya uhamisho wa mchezaji husika katika Mfumo wa Usajili (TMS), licha ya kukumbushwa kufanya hivyo.

Kutokana na uamuzi huo wa FIFA, Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) nalo limeifungia klabu hiyo kufanya usajili kwa wachezaji wa ndani.



You Might Also Like

Get Newsletter

Advertisement