Rais wa Klabu ya Yanga Eng:Hersi Said ameeleza kuwa anaamini mechi walizoalikwa nchini Afrika kusini zitaweza kukijenga na kukitangaza zaidi kikosi kuelekea msimu ujao wa mashindano.

Eng:Hersi amezungumza hayo katika maandalizi ya mwisho kuelekea nchini Afrika Kusini ambapo kikosi kimeshawasiki huku aluyewahinkuwa Straika wa Simba SC Jean Baleke akiwa ni Mmoja wa wachezaji wa Klabu ya Yanga waliokuwa kwenye msafara huo.

Kwa upande wake Kocha wa Klabu ya Yanga Miguel Gamondi ameelezea juu ya Mechi hizo ambazo Moja kwa Moja anaamini zitakuwa na manufaa Kwa kikosi chake huku akielezea ugumu wa Ligi utakavyokiwa kwa msimu ujao kutokana na Kila timu kufanya usajili ulio Bora.

Kwa upande wake Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano Yanga SC Ally Kamwe ameeleza kuwa mialiko hiyo inalenga kukuza zaidi hadhi ya Klabu kwa lengo la kutawala Soka la Afrika.

You Might Also Like

Get Newsletter

Advertisement