Yanga imefuzu hatua ya robo fainali ya michuano ya Kombe la Shirikisho (FA) baada ya kuichapa Dodoma Jiji mabao 2-0 ikiwa kwenye uwanja wake wa nyumbani.

Bao lakujifunga la Emmanuel Martin dakika ya 3 ya kipindi cha kwanza liliifanya Yanga kumaliza kipindi hicho kifua mbele na dakika ya 66 Clement Mnzize akafunga bao la pili, mabao yaliyodumu hadi mwisho wa mchezo, licha ya Dodoma Jiji kukosa penalty waliyoipata kwenye dakika ya 50.

Yanga inaungana na timu zingine saba ambazoni Namungo,Geita Gold, Azam FC, Mashujaa, Ihefu, Coastal Union na Tabora United kufusu hatua ya robo fainali ya michuano hiyo, ikumbukwe Yanga ndiye bingwa mtetezi wa kombe hilo.



You Might Also Like

Get Newsletter

Advertisement