KLABU YA SIMBA YATANGAZA RASMI KUACHANA NA MCHEZAJI WAO NAHODHA JOHN BOCCO
Klabu ya Simba SC imetangaza rasmi kuachana na mchezaji wake na nahodha Mkuu John Bocco baada ya kutoridhishwa na mwendelezo wa ubora wake ingali ameshakuwa kocha wa timu ya vijana ya Simba.
Nyota huyo ameitumikia Simba kwa kipindi cha miaka 7 na anakuwa wa kwanza kupewa THANK YOU katika fagio hilo linalotarajiwa kupita Msimbazi kwenye dirisha hili.
Kabla hata ya msimu kuisha tayari Simba, ilishambadilishia majukumu John Bocco na kumpatia timu ya Vijana ili kuwa kocha mkuu wa timu yao.
John Bocco anatajwa kuwa moja kati ya wachezaji wazawa wenye heshima kubwa haswa mitaa ya Msimbazi, katika ubora wake akiwa na Simba ambapo aliwahi kuwa mfungaji bora wa timu hiyo kwa misimu miwili, pia aliisaidia timu kutwaa ubingwa wa Ligi kuu bara mara nne mfululizo kuanzia mwaka wa 2017-2021,akiipa mataji mawili ya kombe la shirikisho Tanzania Bara, kuifikisha timu hiyo hatua ya robo fainali za kimataifa mara tano, mara 4 Ligi ya Mabingwa na mara moja Kombe la Shirikisho.
Simba wamempa heshima kubwa John Bocco,kwanza kwa kumfanya kuwa nahodha wa timu hiyo alipokuwa uwanjani, pili baada ya kiwango chake kuanza kushuka walimshauri asomee ukocha na kisha wakampatia timu ya vijana chini ya miaka 17 ili ainoe.