KLABU YA SIMBA YAPIGWA FAINI BAADA YA KUJIHUSISHA NA VITENDO VYA KISHIRIKINA KWENYE MCHEZO DHIDI YA MASHUJAA FC
Mechi Namba 166: Simba SC 2-0 Mashujaa FC
Klabu ya Simba imetozwa faini ya Sh. 1,000,000 (milioni moja) kwa kosala mashabiki wake pamoja na walinzi wake wa uwanjani (stewards) kupanga njama na kufanikisha azma ya kuingia uwanjani na kufanya vitendo vinavyoashiria imani za kishirikina wakati mchezo tajwa hapo juu ukiendelea kwenye uwanja wa Azam Complex Machi 15, 2024.
Mashabiki hao walionekana kupitia video fupi iliyosambaa mitandaoni wakijadiliana na mlinzi wa uwanjani (steward) kabla hawajaingia uwanjani kufanya tukio hilo lililoleta taswira mbaya kwa Ligi yetu.
Adhabu hii ni kwa kuzingatia Kanuni ya 47:1 ya Ligi Kuu kuhusu Udhibitikwa Klabu.
Walinzi wa uwanjani (stewards) wa klabu ya Simba, Kessy Mohamed, Mrisho Mindu Pamoja na Mohamed Salmin pamoja na shabiki aliyefahamika kwa jina la Mohamed Saleh, wamefungiwa kuingia viwanjani kwa kipindi cha miezi 12 (kumi na miwili) kwa kosa la kushiriki katika tukio la mashabiki kuingia uwanjani wakati mchezo tajwa hapo juu ukiendelea.
Bodi inaendelea na uchunguzi wenye lengo la kufahamu wahusika wengine wa tukio hilo ambao hawakutambulika mara moja iliwachukuliwe hatua kali za kikanuni.
Adhabu hii ni kwa kuzingatia Kanuni ya 47:2 ya Ligi Kuu kuhusu Udhibitikwa Klabu.
Klabu ya Simba inawajibika kuhakikisha mashabiki na viongozi walioadhibiwa wanatii adhabu zao na kuzitekeleza kikamilifu ili kuepuka