Mara baada ya miaka 23, Klabu ya Pamba FC ya Jijini Mwanza imefanikiwa kupanda kushiriki Ligi kuu msimu wa 2024/25 ikiungana na Kengold ya Jijini Mbeya.

Mara baada ya mafanikio hayo, Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Said Mtanda amezungumza ikiwa ni sambamba na kuweka wazi malengo yao mara baada ya kufanikiwa kumalizika kwa Michuano ya NBC Championship na kufanikiwa kupanda Ligi kuu.


Kwa upande wake Kocha wa Pamba Jiji Fc Renatus Shija ameeleza kuwa mchezo wao wa mwisho dhidi ya Mbui FC ndio ulikuwa karata ngumu kwao katika kuhakikisha wanafikia malengo ya kupanda Ligi kuu.

You Might Also Like

Get Newsletter

Advertisement