Olympiacos imefanikiwa kutwaa ubingwa wa Kombe la Europa Conference League na kuwa timu ya kwanza ya Ugiriki kutwaa ubingwa wa Ulaya.

Olympiacos ilifanikiwa kupata ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Fiorentina kwenye mchezo mkali uliopigwa kwa dakika 120 kwenye Uwanja wa AEK Athens.

Mshambuliaji hatari kwenye timu hiyo, Ayoub El Kaabi alikuwa shujaa kwenye baada ya kufunga bao pekee katika dakika ya 116 ya mchezo huo. Hii ni mara ya pili Fiorentina inapoteza ubingwa wa michuano hiyo katika hatua ya fainali baada ya msimu uliopita kuchapwa na West Ham.

El Kaabi anatajwa kama staa wa timu hiyo msimu huu akiwa alionyesha kiwango cha juu kwenye mchezo wa nusu fainali alipofunga mabao matano peke yake walipovaana na Aston Villa, akiwa amefikisha mabao 33 msimu huu.

"Ni jambo zuri kufanikiwa kucheza mchezo huu na kutwaa ubingwa, bahati nzuri ni kwamba tulikuwa nyumbani na tumefanya kile ambacho mashabiki wetu walikuwa wanataka, tuna mshukuru Mungu kwa hilo," alisema staa huyo baada ya mchezo.

You Might Also Like

Get Newsletter

Advertisement