Ofisa Habari wa Mtibwa Sugar, Thobias Kifaru amesema kwa sasa timu yao ina hali mbaya hivyo anawaomba Watanzania waongeze maombi ili waweze kubaki Ligi Kuu Bara msimu ujao.

Mtibwa imekuwa na mwendelezo wa matokeo mabaya ndani ya uwanja huku Kifaru akisisitiza kuwa tatizo kubwa jingine mbalo bado linawatesa ni kuondoka kwa aliyekuwa Mkurugenzi Mtendaji Mkuu, Jamal Byser.

Mtibwa Sugar imekubali kichapo cha mabao 2-1 kutoka kwa JKT Tanzania kwenye mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara uliopigwa Aprili 29, 2024 kwenye Uwanja wa Meja Jenerali Isamuhyo, Mbweni, Dar es Salaam.

You Might Also Like

Get Newsletter

Advertisement