Manchester United inataka walau asilimia 75 ya kiasi cha pesa ilicholipa kumnunua Jadon Sancho 2021 ikiwa timu yoyote itataka kumsajili mwisho wa msimu huu.

Sancho ambaye alinunuliwa kwa Pauni 75 milioni anadaiwa kuwa katika rada za Borussia Dortmund inayotaka kumsainisha mkataba wa kudumu baada ya ule wa mkopo kumalizika.

Hata hivyo, ili kukamilisha uhamisho wa kutua Dortmund atatakiwa kukubali kupunguza mshahara wa Pauni 275,000 kwa wiki anaoupokea.

Timu nyingi zimeonyesha nia ya kutaka kumsajili Sancho kutokana na kiwango alichoonyesha msimu huu akiwa na Dortmund hadi akaisaidia kufika fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya. Kwa mujibu wa ripoti kocha wa Mashetani Wekundu, Erik Ten Hag hana mpango wa kumtumia staa huyo kwa msimu ujao na amekubali auzwe.

Tangu atue Dortmund, Januari, mwaka huu amecheza mechi 20 za michuano yote, amefunga mabao matatu na ametoa asisti tatu kikiwa ni kiwango bora zaidi kwake.

You Might Also Like

Get Newsletter

Advertisement