KAMATI ya Uendeshaji na Usimamizi wa Ligi ya Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) katika kikao chake cha Februari 19, 2024 ilipitia mwenendo na matukio mbalimbali ya Ligi na kufanya maamuzi yafuatayo;

Ligi Kuu ya NBC

Mechi Namba 121: KMC FC 0-3 Young Africans SC

Klabu ya KMC imepewa Onyo Kali kwa kosa la kuchelewa kwa dakika 15 kufika kwenye kikao cha kitaalam cha maandalizi ya mchezo (MCM) ambapo walipowasili walikuwa hawana vifaa vinavyohitajika jambo lililosababisha kikao hicho kuchelewa zaidi.

Onyo hili ni kwa kuzingatia Kanuni ya 17:2(2.2 & 2.3) na 17:60 ya LigiKuu kuhusu Taratibu za Mchezo.

You Might Also Like

Get Newsletter

Advertisement