Klabu ya Dynamo Basketball ya Burundi kwa mara ya pili yasita kushiriki katika msimu wa BAL (Ligi ya Mpira wa Kikapu Afrika).

Klabu ya Dynamo imeondolewa kwenye Ligi ya Mpira wa Kikapu Afrika baada ya kukataa kuvaa jezi yenye nembo ya 'Visit Rwanda'.

Huku Rais wa Mpira wa Kikapu Afrika, Amadou Gall Fall, akitoa taarifa kuhusu klabu hiyo kushindwa kuzingatia sheria za jezi na sare, imesababisha kufutwa kwa mchezo dhidi ya Petro de Luanda (Angola) na hivyo basi kutoka moja kwa moja kwenye msimu wa BAL 2024 kwa mujibu wa sheria za FIBA.

You Might Also Like

Get Newsletter

Advertisement