Licha ya Chelsea na Arsenal kuonekana zinapambana sana ili kumpata straika wa Newcastle United na Sweden, Alexander Isak, 24, taarifa kutoka tovuti ya Football London zinaeleza kwamba Newcastle haina mpango wa kumuuza staa huyo kwa sasa.

Inaelezwa timu hizi zipo tayari kutoa Pauni 100 milioni iliyodaiwa kuwa ni bei ya Isak ili kumpata.


Awali ilielezwa kwamba Newcastle inataka kumuuza fundi huyu kwa ajili ta kuepuka rungu kutokana na sheria za matumizi ya pesa.

Mkataba wa staa huyu unatarajiwa kumalizika mwaka 2028 na inaelezwa kwamba hana haraka ya kuondoka kwa sasa.

Kwa msimu uliopita alicheza mechi 40 za michuano yote na kufunga mabao 25 hali iliyosababisha timu hizi kuvutiwa naye kiasi cha kutaka kumsajili kutoka na mapungufu iliyo nayo kwenye eneo hilo.

Nyota huyo mwenye asili ya Eritrea, ambaye alizaliwa Sweden, amekuwa na mafanikio makubwa binafsi tangu ametua kwenye Ligi Kuu ya England akitokea katika Ligi Kuu ya Hispania, LaLiga, ambako alikuwa akiitumikia klabu ya Real Sociedad.

You Might Also Like

Get Newsletter

Advertisement