Baada ya kuhukumiwa miaka minne jela kutokana na unyanyasaji wa kijinsia, Barcelona imemuondoa Dani Alves kwenye orodha ya wachezaji waliopewa heshima ya ulijendari wa timu hiyo.

Katika kipindi cha miaka 125 tangu ilipoanzishwa timu hiyo imewapa heshima ya ulijendari wachezaji 102 wakiwemo Jordi Alba, Sergio Busquets na Gerard Pique waliotajwa hivi karibuni.

Kwa mujibu wa tovuti ya Marca, Barcelona imeondoa picha ya staa huyu kwenye tovuti yao ambapo alikuwa amewekwa kama mmoja ya malijendari.

Katika historia yake Alves ndiye mchezaji namba mbili mwenye mafanikio zaidi akiwa na mataji 43 akizidiwa na Lionel Messi pekee.

Akiwa na wababe hao alicheza mechi 408 akashinda mataji matatu ya Ligi ya Mabingwa, matatu ya European Super Cup, matatu ya Klabu bingwa Dunia, sita ya LaLiga, manne ya Copa del Rey na manne ya Supercopa de Espana.

You Might Also Like

Get Newsletter

Advertisement