Barcelona inajiandaa kuwasilisha ofa kwenda Liverpool kwa ajili ya kuipata saini ya staa wa Liverpool na Colombia, Luis Diaz ili kumsajili katika dirisha hili.

Diaz ambaye msimu uliopita alicheza mechi 51 za michuano yote, yeye pia ana ndoto ya kucheza kwenye moja ya timu kubwa ndani ya Hispania.

Mabosi wa Barca wanaamini fundi huyu atawapa mafanikio zaidi akicheza winga wa kushoto ambako kwa sasa anacheza Raphinha.

Mkataba wa Diaz na Liverpool unatarajiwa kumalizika mwaka 2027, lakini kuna uwezekano wakakubali kumuuza ikiwa staa huyo atalazimisha kuondoka.

Diaz ni mmoja kati ya mastaa waliiripotiwa kuwa wanaweza kuachana na majogoo hao baada ya kuondoka kwa Jurgen Klopp mwisho wa msimu uliopita.

Barcelona inaamini Diaz atacheza vizuri katika winga ya kushoto kwa sababu hilo ni eneo lake la asili tofauti na Raphinha ambaye kiasili ni winga wa kulia.

You Might Also Like

Get Newsletter

Advertisement