Arsenal walikuwa na matarajio makubwa wakati timu yao ilipomenyana na Aston Villa lakini uwanja wao ulisalia bila mashabiki dakika 90 baadaye katika mbio za kuwania taji la Ligi Kuu ya Uingereza baada ya matokeo kuchukua mkondo tofauti.

Liverpool walikuwa wa kwanza kujikwaa katika kichapo cha kushtukiza kutoka kwa Crystal Palace kabla ya Arsenal, kulazwa 2-0 na Aston Villa katika uwanja wa Emirates.

Kinyanganyiro cha kushinda ubingwa huo sasa kimekuwa kikali huku kukiwa na pointi mbili pekee zinazotenganisha timu tatu za juu, baada ya manchester City iliokuwa ya tatu katika jedwali kabla ya wikendi kuchukua uongozi baada ya kuilaza Luton 5-1.

Swali kubwa sasa ni je, Arsenal na Liverpool wataimarika kutokana na vipigo hivyo au kasi ya kuwania ubingwa imebadilika kwa upande wa Manchester City?

You Might Also Like

Get Newsletter

Advertisement