Klabu ya Asec Mimosas ya Ivory Coast imeifuata Simba Sc kwenye michuano ya kombe la Shirikisho baada ya kumaliza katika nafasi ya nne kwenye msimamo wa Ligi Kuu Ivory Coast jambo lililofanya washindwe kukata tiketi ya Ligi ya Mabingwa Afrika msimu ujao.

Asec Mimosas waliyopita nyota kama Aziz Ki, Pacome, Yao na Aubin Kramo imemalizika msimu ikifikisha pointi 50 baada ya mechi 30 ikiwa alama 6 tu nyuma ya bingwa Ligi Kuu Nchini humo, San Pedro FC.

Ikumbukwe Asec Mimosas ilikuwa Kundi B sambamba na Simba Sc, Wydad Casablanca na Jwaneng Galaxy kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika msimu uliopita.

Kati ya timu hizo ni Jwaneng Galaxy pekee ambaye atashiriki Ligi ya Mabingwa Afrika msimu ujao.

🇨🇮 ASEC Mimosas ~CAFCL = ❌

🇲🇦 Wydad Athletic ~ CAFCL =❌

🇹🇿 Simba Sports Club ~ CAFCL =❌

🇧🇼 Jwaneng Galaxy ~ CAFCL✅

You Might Also Like

Get Newsletter

Advertisement