Goli pekee lililofungwa na Babacar Sarr dakika ya 77 limeiwezesha Simba SC kutwaa Kombe la Muungano 2024 dhidi ya Azam FC katika Fainali iliyopigwa kwenye Uwanja wa New Amaan Complex, Zanzibar. 

Simba ambayo imekuwa na msimu wa kusuasua katika Ligi Kuu Bara 2023/24 na Ligi ya Mabingwa Afrika 2023/24, kabla ya mchezo huo iliitoa KVZ kwa magoli 2-0 wakati Azam FC iliifunga KMKM magoli 5-2.

Baada ya mchezo huo, Kiungo wa Simba, Saidi Ntibazonkiza 'Saido' aliibuka mchezaji Bora wa Fainali, amesema mashabiki wao hawatakiwi kukata tamaa hata kama timu hiyo inapata matokeo mabaya kwa kuwa ni sehemu ya mchezo. 

You Might Also Like

Get Newsletter

Advertisement