Kiungo wa Yanga SC Stephen Aziz Ki ameshinda tuzo ya Mchezaji bora wa mwezi March kwa kuwashinda Clotous Chama wa Simba SC na Feisal Salum wa Azam FC ambao aliingia nao fainali.

Taarifa ya Bodi ya Ligi imeeleza kuwa Aziz Ki ameshinda tuzo hiyo kutokana na kuwa bora ndani ya mwezi Machi kwa kusaidia timu yake kushinda mechi tatu kati ya nne za Ligi Kuu Bara.


Aziz Ki alicheza jumla ya dakika 330 na amefunga magoli matatu na ametoa pasi za usaidizi wa magoli (assist) 4 (Yanga 5-0 Ihefu, Yanga 1-0 Geita, Namungo 1-3 Yanga na Azam FC 2-1 Yanga).

You Might Also Like

Get Newsletter

Advertisement