KISA CHA IVAN ZAMORANO KUVAA JEZI 1+8 NDANI YA INTER MILAN
Mshambuliaji Ivan Zamorano raia wa Chile alijiunga na Inter Milan mwaka 1996 akitokea Real Madrid.
Alivyofika alikabidhiwa jezi namba 9
Msimu wa 1997 Inter Milan walifanya usajili wa Ronaldo Delima kutoka Fc Barcelona.
Delima alipewa jezi namba 10
Mwaka 1998 Inter Milan walifanya usajili wa kiungo mshambuliaji/ mshambuliaji raia wa Italy Roberto Baggio.
Ujio wa Baggio ulibadilisha kila kitu kwenye matumuzi ya jezi ndani ya Inter Milan.
Baggio alikua akipendelea jezi namba 10,hata timu ya taifa ya Italy ndio jezi aliyokua anaivaaa
Sasa mambo yakawa hivi,Delima ikabidi akabidhi jezi namba 10 Kwa Baggio halafu Ivan Zamorano akaambiwa itabidi jezi namba 9 umpatie Delima.
Nanukuu maneno ya Zamorano, sijachukia kumpa jezi namba 9 Ronaldo, ni mshambuliaji hatari na Mimi ni shabiki yake.
Shida ikaja je Zamorano atavaa jezi namba ngapi?
Alijiuliza maswali mwenyewe na kukosa majibu lakini gwiji wa Inter Milan Sandro Mazzola alimuambia kwanini usivae jezi namba 18? Lakini jezi hiyo katikati ya namba tutaweka alama ya +...
Zamorano aliuliza itawezekana?? Mazzola akamjibu inawezekana bila shida.
Basi ndio jezi hiyo ikatengenezwa na kumfanya Zamorano aonekane nyuma ya mgongo jezi namba 1+8.
Jezi hii iliingia kwenye historia ya soka la Italy kununuliwa zaidi miaka hiyo ya 1998/99.