Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Yanga, Ali Kamwe amesema kikosi cha timu hiyo kinaondoka leo saa 11 jioni kikiwa na jumla ya watu 60.

Akizungumza na waandishi wa habari Kamwe, amesema watasafiri wachezaji 24, benchi la ufundi watu 13 pamoja na viongozi 23.

Yanga inatarajiwa kucheza mchezo wa mwisho wa hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Al Ahly Machi 01, 2024 kwenye uwanja wa kimataifa wa Cairo, Misri

Hata hivyo, timu zote mbili tayari zimefuzu katika hatua ya robo fainali ya michuani hiyo, licha ya kuwa mchezo huo utatoa tathimini ya nani ataongoza kundi D.

You Might Also Like

Get Newsletter

Advertisement