Kikosi cha Mamelodi Sundowns ambacho kinatarajiwa kutua nchini kesho kitakuwa bila nahodha wake Temba Zwene, ambaye hatacheza mchezo wa Jumamosi ijayo.

Mamelodi itatua nchini na zaidi ya watu 70 kwa ajili ya mchezo wa kwanza wa Robo Fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Yanga, utakaopigwa kwenye Uwanja wa Mkapa jijini Dar es Salaam kuanzia saa 3:00 usiku.

Zwena ambaye ni mchezaji muhimu kwenye kikosi hicho hatakuwepo kwenye mchezo huo baada ya kuwa na kadi tatu za njano alizopewa kwenye michezo ya hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

Huyu ni kati ya mastaa wa Mamelodi ambao wamekuwa na heshima kubwa kwenye kikosi hicho alichoanza kukitumikia mwaka 2011, lakini akiwa na historia nzuri ya kupewa kadi kwenye michezo ya ligi pamoja na ile ya kimataifa.

You Might Also Like

Get Newsletter

Advertisement