Mara baada ya kukubali kichapo cha bao 5-0 kutoka kwa Arsenal, Kocha wa Chelsea Mauricio Pochettino amekiri kuwa kikosi chake kilikata tamaa baada ya kuanza kufungwa lakini hanajiimarisha zaidi kwaajili ya mchezo ujao.


Pochettino ameeleza kuwa alizungumza na wachezaji wake katika kipindi cha mapumziko lakini haikuwa bahati kwani walianza vibaya tena katika kipindi cha pili hali iliyowakatisha tamaa wachezaji wake.

Pochettino ameongeza kuwa bado wana uwezo wa kuwa na uchezaji mzuri na siku tatu baadaye, na wanaamini wataonyesha viwango vya juu.


Chelsea watakuwa ugenini kumenyana na Aston Villa siku ya Jumamosi, huku Arsenal wakicheza na wapinzani wao wa London kaskazini Tottenham Hotspur siku ya Jumapili.

You Might Also Like

Get Newsletter

Advertisement