Klabu ya Tabora United imemtambulisha rasmi kocha mpya, Denis Laurent Goavec raia wa Ufaransa kurithi mikoba ya Goran Copunovic masaa matatu tu baada ya kufikia makubaliano ya pande mbili.

Kocha huyo mwenye umri wa miaka 66 amesaini mkataba hadi mwishoni mwa msimu huu 2023/2024 ikiwa timu hiyo imebakiza mechi tisa tu kumaliza msimu.

Goavec mwenye leseni ya Shirikisho la Soka barani Ulaya (UEFA Pro Licence) ameshafundisha soka barani Afrika katika klabu za As Vita ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Js Soura ya Algeria na timu ya taifa ya Benin.

Mfaransa huyo ana kibarua cha kuisaidia timu hiyo kumaliza katika nafasi nzuri kwenye msimamo wa Ligi kwenye mechi zilizobaki, kwani kwa sasa inashuka nafasi ya 13 na pointi 21 ikiwa imecheza mechi 21.

Kibarua cha kwanza cha Goavec baada ya kutua Tabora United kitakuwa Aprili 4, 2024 katika mchezo wa Kombe la Shirikisho la Azam (ASFC) hatua ya 16 bora dhidi ya Singida Fountain Gate katika Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.





You Might Also Like

Get Newsletter

Advertisement