KAULI YA MANGUNGU NA CEO WA SIMBA LEO
"Tupo imara, kila Mwanasimba atekeleze majukumu ili tufikie malengo yetu na kufikia hatua nzuri. Sandaland amekuwa mfano mzuri wa kazi anayofanya, mdhamini mkuu M-Bet, makampuni ya Mo na wadhamini wengine wote."- Mwenyekiti wa klabu, Murtaza Mangungu
"Sisi tujione kuwa watu wenye bahati kubwa kushiriki na kuzindua African Football League kwa timu zote nane ambazo zitashiriki michuano hii."- CEO Imani Kajula