KASONGO: KAMA AL HILAL NI WASHIRIKI WA LIGI KUU BARA MSIMU UJAO NI FAIDA KWA KLABU ZA TANZANIA
Mkurungezi wa Bodi ya Ligi, Almas Kasongo amekiri klabu ya Al Hilal Omdurman ya Sudan imeomba kuwa sehemu ya Ligi Kuu Bara.
Amesema hilo linawezekana kwa sababu ni jambo ambalo linazungumzika kutokana na hali ya kiusalama nchini Sudan kwa sasa.
Hata hivyo, ameongeza kama Al Hilal washashiriki msimu ujao faida ni nyingi kwa klabu za Tanzania kuliko chagamoto kutokana na uzoefu wa timu hiyo kushiriki mara kwa mara michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika na Kombe la Shirikisho.
Pia amesema kuna baadhi ya waamuzi kutoka Sudan watakuwa miongoni mwa watakochezesha mechi za Ligi Kuu Bara msimu ujao 2024/2025.