Mchezaji wa Al Ittihad, Karim Benzema (36) alifunga bao la haraka zaidi katika historia ya Saudi Super Cup na kusaidia timu yake kupata ushindi wa 2-1 dhidi ya Al Wehda mjini Abu Dhabi siku ya Jumatatu na kutinga fainali.

Benzema alifunga goli ya sekunde 55 na kuvunja rekodi ya mshambuliaji wa Al Fateh Doris Salomo Fuakuputu iliyowekwa kwenye fainali ya kwanza mwaka wa 2013.

Goli hilo lilikuwa bao la kwanza la mshambuliaji huyo wa Ufaransa mwaka 2024.

Kocha wa Al Ittihad, Marcelo Gallardo atakuwa anatazamia kunyanyua taji lake la kwanza kwa klabu hiyo katika fainali itakayopigwa Alhamisi hii dhidi ya Al Hilal ambao wamewaondoa Al Nassr katika hatua ya nusu fainali.

You Might Also Like

Get Newsletter

Advertisement