Yanga imeanza kupiga hesabu za mchezo wake dhidi ya Simba 'Dabi ya Kariakoo' ambapo jana iliamua kutowatumia nyota wake watatu waliokuwa majeruhi, Pacome Zouzoua na Yao Attohoula dhidi ya Dodoma Jiji na kumpa Khalid Aucho dakika chache kwe mechi hiyo ikilenga kuwatumia katika mechi dhidi ya watani wao, Aprili 20 kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam.

Watatu hao tayari wameshapona majeraha yaliyokuwa yakiwakabili na wameshaungana na wenzao katika program za mazoezi lakini hawatotumika kwa mechi za hivi karibuni ili kutowaweka katika hatari ya kuikosa Simba.

"Tuna mchezo muhimu dhidi ya Simba hapo Aprili 20 ambao tunahitaji kupata ushindi wa kishindo ambao utatuweka katika nafasi nzuri ya kutwaa ubingwa na hili hilo litimie tunapaswa kuwa na hao watatu hivyo ndio maana kwa sasa tunawaandaa kimyakimya ili waje kuionyesha kazi Simba," amesema mmoja wa viongozi wa timu hiyo.

Kamwe amesema kuwa watatu hao wamesharejea kikosini na wanaendelea vizuri na maandalizi ya kuivaa Simba katika mchezo ambao wamepania kupata ushindi kwa sababu tatu kubwa.




You Might Also Like

Get Newsletter

Advertisement