KAMATI YA OLIMPIKI (IOC) IMETANGAZA WANARIADHA WATAKAO SHIRIKI KWENYE OLIMPIKI YA WAKIMBIZI PARIS 2024
Kamati ya Olimpiki ya Kimataifa (IOC) imetangaza wanariadha ambao watakuwa sehemu ya Timu ya Olimpiki ya Wakimbizi ya IOC kwenye Michezo ya 2024 huko Paris, Ufaransa.
Wanariadha hao 36 wanatoka nchi 11 tofauti ambapo wamechaguliwa kulingana na utendaji wao wa michezo na hali ya mkimbizi iliyothibitishwa, lakini fikira pia imezingatiwa kusawazisha uwakilishi katika michezo, jinsia na nchi.
Wanariadha hao wameandaliwa na Kamati za Kitaifa za Olimpiki (NOCs) kote ulimwenguni huku wanashindana katika michezo 12, ikiwa ni pamoja na baiskeli barabarani, ambayo kuna washiriki wawili.
Eyeru Gebru mwendesha baiskeli wa barabarani kutoka Ethiopia ambaye amewakilisha nchi yake kwenye michuano mikubwa, ikiwa ni pamoja na kutwaa nafasi ya pili katika mbio za barabarani kwenye Mashindano ya Bara la Afrika mwaka 2019, atawakilisha timu katika mbio za baiskeli barabarani za wanawake.
Kwa sababu ya vita vya wenyewe kwa wenyewe kaskazini mwa Ethiopia mnamo 2021, Gebru amehamia Ufaransa, ambapo sasa anaishi. Anakimbilia timu ya Continental Komugi-Grand Est.
Amir Ansari atawakilisha timu katika mbio za barabara za wanaume. Ansari alizaliwa nchini Iran na kukulia Afghanistan, lakini alilazimika kukimbia mwaka wa 2015. Alitafuta hifadhi nchini Sweden ambako anaishi sasa. Ameshindana kama sehemu ya timu ya Stockholm CK na Timu ya Wakimbizi ya UCI.
Timu nzima ya wakimbizi inaongozwa na mwendesha baiskeli Masomah Ali Zada ambaye alishindania timu ya wakimbizi huko Tokyo 2020 na sasa ametunukiwa jukumu la Chef de Mission kwa Timu ya Olimpiki ya Wakimbizi.
IOC ilianzisha timu ya wakimbizi katika Mkutano Mkuu wa Umoja wa Mataifa mwaka 2015 ambapo timu ya kwanza ya Wakimbizi ya Olimpiki, iliyojumuisha wanariadha 10, ilishiriki katika Michezo ya 2016 huko Rio huku Olimpiki ya Mwaka 2020 iliyofanyika Tokyo ikishirikisha wanamichezo 29.
Rais wa IOC Thomas Bach alizungumzia chimbuko la timu kwenye tangazo hilo na kueleza kuwa Ilikuwa muhimu kuianzisha kwa la kuwasaidia wanamichezo sambamba na kuwa na ongezeko la wanamichezo.
Pia aliangazia umuhimu unaoendelea wa mpango huo huku idadi ya wakimbizi ikiendelea kuongezeka na kuongeza wanatarajia hadi mwishoni wa mwaka huu karibu watu milioni 130 waliokimbia makazi na wahamiaji hivyo ilikuwa ni lazima kabisa kuendelea na hata kuimarisha programu ya sasa kwaOlimpiki ya Paris 2024.