KAMATI YA BUNGE ITAWASILISHA MAPENDEKEZO JUU YA UWANJA MPYA WA ARUSHA KUTAMBULIKA KWA JINA LA SAMIA SULUHU HASSAN
Uwanja wa Mkapa ulijengwa kwa ushirikiano wa Serikali ya Tanzania na China ukigharimu Dola za Marekani Milioni 56 (Tsh. Bilioni 64 kwa Mwaka 2007).
Mpango uliopo sasa ni mchakato wa ujenzi wa uwanja mwingine Mkoani Arusha ambao Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Elimu Utamaduni na Michezo imesema itawasilisha mapendekezo utambulike kwa jina la Uwanja wa Samia Suluhu Hassan.
Pia, Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo imesema mipango iliyopo ni kuwa mradi huo utakaojengwa kwa Dola Milioni 112 (Tsh. Bilioni 286) kabla ya kodi, ukamilike kabla ya Mwaka 2027 ili utumike katika Michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON).