Beki wa Coastal Union, Lameck Lawi amefutiwa kadi nyekundu aliyopewa kwenye mchezo wao dhidi ya Yanga, uliochezwa Aprili 27, 2024 kwenye Uwanja wa Azam Complex Chamazi.



Lawi amefutiwa kadi hiyo baada ya Kamati ya Uendeshaji wa Ligi kupokea taarifa za uchambuzi wa kitaalamu kutoka kwa wakufunzi wa waamuzi ambazo ziliainisha kuwa mchezaji huyo hakustahili kuonywa kwa kadi nyekundu badala yake alipaswa kuonywa kwa kadi ya njano kwani kulikuwa na mlinzi mwingine wa Coastal ambaye angeweza kufikia mpira.

Lawi alipewa kadi nyekundu baada ya kumvuta jezi Aziz KI wakati wakipambania mpira uliokuwa ukielekea kwenye lango la Coastal Union.

Maamuzi hayo yamezingatia kanuni ya 12:8 ya Ligi Kuu kuhusu usimamizi wa Ligi.

Aidha kamati imesema kuwa, Mwamuzi wa kati na msaidizi wa mchezo huo wamepewa onyo kali kwa kosa la kushindwa kutafsiri sheria za mpira wa miguu katika tukio hilo.

Uamuzi umetolewa kwa kuzingatia kanuni ya 42:1 (1, 1) ya Ligi Kuu kuhusu uthibiti wa waamuzi.

Katika mchezo huo Yanga ilishinda bao 1-0 lililofungwa na mshambuliaji Joseph Guede







You Might Also Like

Get Newsletter

Advertisement