Rasmi klabu ya JS Kabylie ya Algeria imechana na mshambuliaji Mtanzania Simon Msuva.

Katika taarifa yake Kabylie mbali na Msuva pia imeacha na mshambuliaji mwingine mkongwe Hichem Mokhtar raia wa Taifa hilo. Msuva aliyejiunga na klabu hiyo Agosti

27,2023 akitokea Al - Qadsiah ya Saudi Arabia hakufanikiwa kuwa mwanzo mzuri ndani ya timu hiyo kwa kukosa kuanza kwenye mechi nyingi na Waalgeria hao.

Ujio wa kocha Mreno Lui Almeida umechangia kwa kiasi kikubwa kuondoka kwa Msuva ndani ya Kybalie baada ya kocha huyo kushindwa kukubaliana na uwezo wa mshambuliaji huyo wa zamani wa Yanga.

Almeida amewaambia mabosi wa Kabylie kuwa anataka washambuliaji wengine wawili wenye makali zaidi tofauti na hawa ambaoa emewatema. Inaelezwa kocha huyo amewapendekeza wachezaji wawili kutoka Ureno akitaka wasajiliwe na Kabylie haraka.

You Might Also Like

Get Newsletter

Advertisement