Mara baada ya kufanikiwa kubeba Kombe la FA Tanzania Bara Nahodha msaidizi wa Klabu ya Yanga ameweka wazi juu ya deni walilonalo kwa mashabiki kuhakikisha msimu ujao wanafanya vizuri zaidi ya msimu huu.

Job ameeleza kuwa maandalizi mazuri kwaajili ya kuelekea msimu ujao sambamba na kuweka nguvu ya pamoja wanaamini watatetea kila walichokichukua kwa msimu huu.

“Deni kwa mashabiki wetu kwaajili ya msimu ujao tutalilipa kwa kufanya maandalizi mazuri na tukiweka nguvu kwa pamoja na maandalizi mazuri tutaweza kukitetea kwa kila tulichi=okichukua kwa msimu huu, ” Amesema Dickson Job – Mchezaji Yanga SC.

Job ameweka wazi kuwa mchezo dhidi ya Azam FC haukuwa na ugumu katika kupambana kutokana na kila mchezaji kuelewa umuhimu na uhitaji wa timu katika mchezo huo.

“Kwenye michezo kama hii huwa hakuna ugumu sana kama mkicheza michezo midogo kwamaana mkicheza michezo midogo morali ya mchezaji inakuwa chini lakini unapofikia katika hatua hii kwa maana ya mchezo mkubwa na ukizingatia ni wa Fainali kila mchezaji anaelewa umuhimu wa mchezo huo na uhitaji wa timu katika mchezo huo kwahiyo unakuwa ni mchezo rahisi sana kuweza kuongea na wachezaji wenzako na kuweza kupambana kupata matokeo, ” Amesema Dickson Job – Mchezaji Yanga SC

Job ameongeza kuwa licha ya kufika katika dakika za nyongeza na hatimaye katika changamoto za Mikwaju ya Penati katika mchezo huo wa Fainali ya FA dhidi ya Azam FC uliopigwa Uwanja wa New Amaan Complex, wao kama wachezaji haikuwapa presha kwani walishazoea kutokana na michezo mbalimbali kupitia katika hatua hiyo ikiwemo michezo ya Kimataifa.

You Might Also Like

Get Newsletter

Advertisement