Klabu ya JKT Tanzania imefanikiwa kusalia kwenye ligi kuu ya NBC Tanzania bara kufuatia ushindi wa jumla ya mabao 4-0 dhidi ya Tabora United kwenye michezo miwili ya ‘playoff’.


Mchezo wa mkondo wa kwanza uliopigwa katika dimba la Ali Hassan Mwinyi Tabora uliishuhudia JKT Tanzania ikishusha kipigo cha 4-0 kabla ya kutoshana nguvu kwa sare tasa katika dimba la Meja Jenerali Isamuhyo Dar.


Hivyo kwa matokeo hayo Tabora United watalazimika kucheza mechi mbili za ‘playoff’ dhidi ya Biashara United ili kujitetea.

You Might Also Like

Get Newsletter

Advertisement