Wawakilishi wa Tanzania kunako Michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika kwa Wanawake, JKT Queens wamepangwa Kundi A kwenye Michuano hiyo itakayoanza kutimua vumbi Novemba 05 mwaka huu nchini Ivory Coast.

JKT Queens imepangwa kundi moja na wenyeji Athletico FC D,Abidjan, Sporting Casablanca ya Morocco na Mabingwa watetezi wa michuano hiyo Mamelody Sundowns ya Afrika Kusini huku Kundi B likiwa na timu za AS FAR ya Morocco, Ampen Darkoa ya Ghana, Huracanes FC ya Equatorial Guinea na AS Mande ya Mali.

Michuano hiyo itachezwa katika Viwanja vya Laurent Pokou jijini San Pedro na Amadou Gon Coulibaly jijini Korhogo

You Might Also Like

Get Newsletter

Advertisement