Hakuna asiyejua kuhusu kadi nyekundu ama kadi ya njano katika mchezo wa soka. Kwa wengi wanaofuatilia soka, kadi nyekundu inafahamika zaidi kwa kuwa hupewa mchezaji ambaye aameonyesha mchezo usio wa kiungwana kama kucheza rafu mbaya, kushika mpira kwa makusudi, kutukana na mengine. Inawahusu pia hata benchi la ufundi.

Kadi ya njano yenyewe inatumika kuonya mchezaji ama bechi la ufundi ama yeyote anayehusishwa na mchezo kwa makosa madogo madogo ya uwanjani ama nje ya uwanja.

Kadi hizi zilianza kutumika miaka zaidi ya 50 iliyopita ikitambulishwa kwa mara ya kwanza kwenye kombe la dunia la mwaka 1970 lililofanyika nchini Mexico ili kupunguza rafu uwanjani zilizoanza kuongezeka katika mechi nyingi za soka wakati huo.

Lakini Januari 21, 2023 imekuwa siku ya kihistoria kwa kadi nyingine ya tatu kuanza kutumika, ni kadi nyeupe.

Imeanza kutumika rasmi kwa mara ya kwanza katika historia ya soka duniani kwenye mchezo wa kombe la ligi huko Ureno kwa timu za wanawake kati ya Sporting Lisbon na Benfica.

Rangi nyeupe ina maana na uhusiano kadhaa wa kadhaa, ingawa maana zinaweza kutofautiana kulingana na mtu binafsi na tamaduni wanazoishi nazo.

Lakini tafsiri isiyo rasmi kuhusu rangi nyeupe iliyozoeleka mara nyingi rangi nyeupe inawakilisha usafi, kutokuwa na hatia na unyenyekevu.

Hili la unyenyekevu ndilo hasa linalohusisha kwa namna yake kadi nyeupe iliyoanza kutumika katika mchezo wa soka duniani.

Kadi nyeupe inaonyeshwa kutambua na kuhamasisha 'fair play' au uungwana, mchezo mzuri ama jambo zuri katika mchezo wa soka na "imewekwa maalumu kuboresha na kuimarisha nidhamu katika mchezo wa soka", anasema Shaban Shomvi, mmoja wa wacheza soka wa zamani wa Tanzania.

Huko nyuma mchezo mzuri ama jambo zuri la kiungwana katika mchezo huo lilitambuliwa baadaye kwa tuzo kutolewa kwa timu fulani ama mchezaji ama mdau yeyote wa soka, lakini sasa kadi hii itaanza kutambua hilo hapo hapo uwanjani wakati mchezo ukiendelea.

Sporting Lisbon na Benfica ni timu hasimu nchini Ureno, ziwe zinakutana timu za wanaume ama wanawake, mechi baina ya timu hizi huwa na upinzani mkali na wakati mwingine uleta vurugu ndani na nje ya uwanja.

Pengine muamuzi Catarina Camposwa aliyechezesha mchezo huo uliozikutanisha timu hizi katika mchezo wa robo fainali ya Taca de Portugal cup kwa wanawake uliopigwa Januari 21, 2023 mjini Lisbon aliona umuhimu wa kuwa nayo na kuitoa kwa sababu ya asili ya upinzani uliopo. Lakini kwa aina ya mchezo huo kuyapata matukio ya 'kiutu' yanayostahili kadi nyeupe iliwezekana.

Mchezo ukiwa unaendelea mmoja wa mashabiki alijisikia vibaya' kuumwa', ikalazimu madaktari wa timu zote mbili kukimbilia jukwaani kumsaidia kuokoa maisha ya mgonjwa huyo, kitendo hicho kilionekana ni cha kiungwana, kimichezo na cha kiutu, kilichomfanya refa au muamuzi Camposwa kuwapa kadi hiyo nyeupe madaktari wa pande zote mbili. Historia ikaandikwa.

Benfica ilishinda mchezo huo kwa mabao 5-0 mjini Lisbon. Lakini ushindi huo wala sio jambo linalozungumzwa, kinachozungumzwa ni kadi nyeupe na uungwana wa madaktari hao wa timu hizo. ilishinda mchezo huo kwa mabao 5-0 mjini Lisbon. Lakini ushindi huo wala sio jambo linalozungumzwa, kinachozungumzwa ni kadi nyeupe na uungwana wa madaktari hao wa timu hizo.

You Might Also Like

Get Newsletter

Advertisement