Jesca Mfinanga na Egine Kayange, wameondoka nchini asubuhi ya leo Alhamisi kwenda Afrika Kusini kwa ajili ya pambano tofauti.

Wakiwa Afrika Kusini, Jesca anatarajia kucheza pambano kuu la kuwania Mkanda wa Ubingwa wa Afrika dhidi ya Simangele Hadebe raia wa nchi hiyo.

Jesca mwenye umri wa miaka 25 ana rekodi ya kucheza mapambano manane, akishinda matano likiwamo moja la KO, kupoteza mawili bila ya kupigwa KO bna pambano moja kumalizika kwa sar, huku mpinzani wake Simangele ana rekodi ya kucheza mapambano 18, akishinda 13 kupoteza matatu na kutoka sare mbili.

Katika mapambano hayo 13, Msauzi huyo ameshinda manne kwa KO, huku akipoteza moja tu kwa KO kati michezo mitatu aliyopigwa, kitu kinachoonyesha pambano dhidi ya Jesca litakuwa ngumu kwa pande zote mbili, japo Mtanzania ametamba anataka ubingwa wa Afrika.

Kwa upande wa Egine, atapanda ulingoni katika pambano la utangulizi dhidi ya Monica Mukandla kutoka Zimbabwe.

Mapambano hayo yanatarajiwa kupigwa Jumamosi ya Juni 22 kwenye Ukumbi wa Klip Livierbeg Creation Centre nchini humo.

You Might Also Like

Get Newsletter

Advertisement