JEAN LOUIS AJIUZULU IVORY COAST
Timu ya taifa ya Ivory Coast imethibitisha kuachana na kocha wao mkuu Jean-Louis Gasset ambaye amejiuzulu wakati mashindano ya AFCON 2023 yakiwa bado yanaendelea.
Timu ya taifa ya Ivory Coast tayari imefuzu hatua ya 16 bora na itakua chini ya Emerse Faé ambaye anakaimu nafasi hiyo ya kocha mkuu kwa muda.