KOMPANY anatajwa kuwa katika hatua za mwisho kuwa kocha mpya wa Bayern baada ya kuondoka kwa Thomas Tuchel mwishoni mwa msimu huu.

Kocha huyo raia wa Ubelgiji aliiongoza Burnley kunyakua taji la Ligi Daraja la Kwanza msimu wa 2022/23, licha ya kushinda kuibakisha Ligi Kuu msimu ujao.

Anahitaji huduma ya Grealish ili kujenga upya timu eneo la kiungo na ushambuliaji na anaamini staa huyo anafaa.

Bayern inaamini kuna uwezekano mkubwa wa kumpata Grealish kwa kumtumia Harry Kane ambaye anaweza akamshawishi, pia mafanikio ya Jadon Sancho aliyopata muda mfupi baada ya kurejea Dortmund yanatajwa huenda ikawa ni kishawishi kwake.


Msimu huu Grealish, 28, alicheza zaidi ya dakika 1000 za katika mechi za Ligi Kuu England na kuisaidia Man City na kushinda taji la kihistoria la nne mfululizo.

Alicheza mechi zote za robo fainali ya Ligi ya Mabingwa dhidi ya Real Madrid.

Kwa takwimu za michuano yote staa huyu amefunga mabao matatu na asisti tatu katika mechi 36.

Mechi nyingi za EPL amekuwa akianzia benchi na Guardiola anaonekana kuwatumia zaidi Jeremy Doku na Phil Foden katika eneo lake.

Licha ya kutomchezesha kama ilivyokuwa msimu uliopita ripoti kutoka The Mirror zinaeleza kwamba Guardiola bado ni shabiki mkubwa wa staa huyu na bado anaamini anamhitaji katika timu.

Licha ya kiwango chake, Grealish ameitwa katika kikosi cha timu ya taifa ya England kitakachoshiriki michuano ya Euro inayoanza Juni 16 mwaka huu.

You Might Also Like

Get Newsletter

Advertisement