JA MORANT KUKOSEKANA MSIMU HUU WA NBA
Mchezaji wa kikapu nyota wa Memphis Grizzlies Ja Morant atafanyiwa upasuaji, kuhitimisha msimu wake, kama ilivyotangazwa Jumatatu usiku. Alitolewa kwenye mechi ya Jumanne dhidi ya Dallas Mavericks kutokana na maumivu ya bega la kulia.
Uamuzi huu wa kufanyiwa upasuaji ulifanyika baada ya Morant kupata kulegea katika bega lake la kulia alipokuwa akifanya mazoezi siku ya Jumamosi, na kusababisha akose nafasi kenye ushindi wa Grizzlies dhidi ya Phoenix Suns na anatarajiwa kukaa nje mpaka mwisho mwa msimu.