Iron Biby, jina lake halisi Cheick Ahmed Al-Hassan SANOU, ni bingwa wa dunia wa kubeba chuma, amebeba kilo 230.

Raia huyo wa Burkina Faso, alizaliwa akiwa na uzito wa kilo 5 katika mji wa Bobo-Dioulasso, nchini humo.

Iron Biby anashikilia rekodi muhimu zaidi duniani zinazohusisha na kuinua uzito zinazomfanya mnyanyuaji bora zaidi katika historia.

Ufanisi huo umemfanya Iron Biby kutunukiwa heshima na kiongozi nchini humo Kapteni Ibrahim Traore kwa kuiletea nchi hiyo sifa.

Iron Biby pia ndiye mtu mwenye mikono kubwa zaidi duniani.

Iron Biby amekuwa chanzo cha motisha Burkina Faso nzima, akionyesha kwamba nguvu na ujasiri unaweza kushinda vikwazo.

You Might Also Like

Get Newsletter

Advertisement