Mshambuliaji Lionel Messi amejitetea baada ya mashabiki wa huko Hong Kong kuwazomea Inter Miami kwa sababu alikosa mechi ya kirafiki ya kujiandaa na msimu mpya.

Inter ilishinda Ligi XI 4-1 mbele ya karibu mashabiki 40,000 siku ya Jumapili, huku nahodha wa Argentina Messi akiachwa kwenye benchi kwa sababu ya tatizo la misuli ya paja.

Serikali ya Hong Kong ilisema Messi alipewa kandarasi ya kucheza angalau dakika 45.

“Siku zote huwa natamani kucheza, hasa katika michezo hii ambayo tunasafiri mbali na watu wanataka kuona michezo yetu,” alisema.

"Kwa bahati mbaya hii hutokea katika soka. Katika mchezo wowote inaweza kutokea kwamba huwezi kucheza.

"Natumai tunaweza kurudi na kucheza mchezo huko Hong Kong."

Wafuasi katika umati wa karibu wa watu 38,323 katika Uwanja wa Hong Kong walilipa zaidi ya HK$1,000 (£101) kwa tikiti.

You Might Also Like

Get Newsletter

Advertisement