Rais wa Club ya Yanga Injinia Hersi Said ameishukuru Serikali kupitia Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo baada ya kukubali ombi la Club hiyo la kusafirisha na kuwagharamia kila kitu Mashabiki 48 kwenda South Africa kuishangilia Yanga kwenye mechi yake ya marudiano na Mamelodi Sundowns Ijumaa hii.

“Niwatakie safari njema na nina imani safari yetu ya kurudi itakuwa nzuri kwakuwa tutarudi tukiwa tayari tumeshafuzu hatua ya nusu Fainali, Wizara itahudumia gharama zote za safari ya kuelekea Afrika kusini yenye Wanachama na Mashabiki wetu 48 kuanzia nauli mpaka pesa ya kujikimu, Yanga tunaishukuru sana Wizara”

“Hapo mwanzo tulitangaza Watu watakaosafiri walipaswa kuwa na shilingi laki 6 na tulipata Watu 30, niwahakikishie baada ya Wizara kukubali kusafirisha Wanachama na Mashabiki wetu, zile laki 6 zitarudishwa kwa wenyewe” amesema Hersi.



You Might Also Like

Get Newsletter

Advertisement