IMRAN KHAN NAHODHA WA ZAMANI WA TIMU YA TAIFA PAKISTAN AHUKUMIWA JELA MIAKA 10
NAHODHA wa zamani wa timu ya taifa ya Kriketi na Waziri Mkuu wa zamani wa Pakistani, Imran Khan, amehukumiwa kwenda jela kwa kipindi cha miaka 10 baada ya kukutwa na hatia kwenye kesi ya uvujishaji wa nyaraka za serikali.
Khan, alienguliwa nafasi yake ya uwaziri mkuu mwaka 2022, tayari anatumikia adhabu ya kifungo cha miaka mitatu jela kwa kesi nyingine ya rushwa.
Mwenyewe amejitetea kuwa kesi zote zinaendeshwa kisiasa, ikiwa zimebaki siku chache kuelekea uchaguzi mkuu, huku akiwataka wapakistani kuitumia nguvu ya kuchagua wanaemtaka kwa maslahi ya nchi.